ADVERTISEMENT
TANGAZO LA ZABUNI YA UJENZI WA MAJENGO YA KITUO
CHA MAFUNZO YA KILIMO MSETO, BAHI, DODOMA
Mwisho kupokea maombi: Tarehe 09 Juni 2024
Inades-Formation Tanzania (IFTz) ni Shirika Lisilo la Kiserikali lenye makao yake makuu Area C Jijini Dodoma. Tunakaribisha zabuni ya ujenzi wa majengo katika kituo cha mafunzo ya kilimo-mseto—Dryland Agroforestry Training Centre—kama ifuatavyo:
- Ujenzi wa Ofisi ya Kituo (Ukubwa wa chumba uwe ni 4mx5m)
- Ujenzi wa nyumba (Yenye vyumba 2 vya kulala, sebule, choo, bafu, jiko kwa pamoja) 3) Ujenzi wa Choo (Jengo moja lenye mgawanyo wa sehemu mbili (Kiume na Kike). Upande wa Kike kuwe na vyoo 2 (choo moja ya kukaa na nyingine ya kuchuchumaa) na upande wa Kiume kuwe na vyoo 2 (choo moja ya kukaa na nyingine ya kuchuchumaa).
- Ujenzi wa Jiko (Lenye ukubwa wa 4mx4m).
- Ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano/Darasa (Wenye uwezo wa kuchukua watu 60 waliokaa kwa wakati mmoja
- Ujenzi wa mnara wa tenki la maji (Lenye kuezekwa kwa zege (concrete slab) lenye uwezo wa kubeba Simtank 2 zenye ujazo wa Lita 5,000 kila moja au Simtank 1 lenye ujazo wa Lita 10,000 za maji)
- Jukwaa la wazi (Open-air stage/theatre).
- Lango Kuu lenye upana wa 6m na urefu wa 7m (Main entrance gate branded). Kwa sasa litakuwa na nguzo nne (mbili kila upande) zitakazoshikilia ubao wenye maandishi
“DRYLAND AGROFORESTRY TRAINING CENTRE (DATC) ESTABLISHED BY INADES-FORMATION TANZANIA IN PARTNERSHIP WITH VI AGROFORESTRY
Kazi ya ujenzi wa majengo haya itafanyika katika eneo la kituo cha Mafunzo ya Kilimo Mseto kwenye eneo Kame, lililopo Kitongoji cha Lulunde katika makutano ya vijiji vya Kisima cha ndege, Zanka na Asanje Wilaya ya Bahi, Kilomita 45 kutoka Dodoma Mjini.
Sifa zinazotakiwa kwa waombaji:
- Iwe ni kampuni au mtu binafsi aliyesajiliwa Kufanya kazi za ujenzi.
- Awe na uwezo wa kuchora ramani za majengo, na kuandaa makadirio ya gharama za mahitaji ya ujenzi wa majengo (Bill of Quantity-BoQ) na kusoma ramani za majengo.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa ubora na kuikamilisha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano.
- Awe mlipa kodi na anayeweza kutoa risiti ya mashine za EFD.
- Mwenye uwezo wa kufanya kazi na kuikamilisha kwa kulipwa kwa awamu na kupokea malipo ya mwisho baada ya kukabidhi kazi iliyofanyika.
- Mwenye uzoefu wa shughuli za ujenzi usiopungua miaka 4.
- Maelezo mafupi ya kampuni au sifa zake zinazoelezea uzoefu kwenye kazi za ujenzi ambatainisha na vyeti/leseni halali za kufanya kazi.
- Uteuzi wa mzabuni utazingatia uzoefu na gharama za ufanyaji kazi husika kwa kipindi kilichokubaliwa.
Kwa wale wenye sifa na vigezo tajwa hapo juu wanaombwa kutuma au kufika ofisi za Inades Formation Tanzania, zilizopo Dodoma eneo la Area C, kuleta au kutuma barua za maombi kupitia anuani hii:
Mkurugenzi Mtendaji,
Inades Formation Tanzania-IFTz, S.L.P 203, Area C, Dodoma.
Barua pepe: inadesformation.tanzania@inadesfo.net
Nakala ya Barua pepe: mbarwa.kivuyo@inadesfo.net
Download the Advertisement